Ticker

6/recent/ticker-posts

Kagere Kurejesha Majeshi Rwanda Baada ya Tetesi za Kuachwa na SimbaBAADA ya kuwa na uhakika wa kutoendelea kukipiga Simba, klabu ya Kiyovu inayoshiriki Ligi Kuu Rwanda, imeanza kumnyatia mshambuliaji Meddie Kagere ili kuongeza nguvu eneo la ushambuliaji msimu ujao.

Kiyovu ni kati ya klabu alizowahi kuzichezea mara kadhaa miaka ya nyuma alipokuwa nchini Rwanda alikopewa uraia, licha ya asili yake kuwa ni Uganda.

Kagere ni kati ya wachezaji wanaotajwa kuwa mbioni kutemwa na Simba kwa msimu ujao kutokana na kushindwa kufanya maajabu, licha ya kufunga mabao saba na kuasisti mara mbili msimu huu.

Nyota huyo wa kimataifa wa Rwanda, anamaliza mkataba wake Msimbazi, klabu aliyojiunga nayo misimu minne iliyopita na kuifungia mabao ya kutosha ikiwamo kubeba tuzo ya Mfungaji Bora wa Ligi Kuu mara mbili mfululizo 2018-19 na 2019-20 akifunga mabao 23 na 22.


Msimu wa 2020-21 kasi yake ilipungua na kumaliza na mabao 13 akishika nafasi ya tatu ya wafungaji bora wa msimu na safari hii kuporomoka zaidi, jambo lililoufanya uongozi kupiga hesabu za kumpiga chini na kuleta nyota wengine wapya wa kuirejeshea makali timu hiyo kwa msimu ujao.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments