Kajala na Harmonize Wapania Kufanya Kufuru, Waanza na Qatar na Dubai

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




MSANII wa Bongo Movies ambaye pia ni mpenzi na Meneja wa Harmonize, Kajala Masanja ameanza rasmi majukumu yake ya umeneja wa Harmonize ambapo miongoni mwa vitu alivyoanza navyo ni kushiriki music video ya staa huyo.

Licha ya hilo, Kajala ameongozana na Harmonize katika shoo zake mbili zinazotarajiwa kufanyika moja ni Doha, Qatar na nyingine Dubai.


Harmonize
Harmonize ataanza na shoo ya Doha iliyopewa jina la The Ultimate Shutdown Afro Bongo Night ambayo itakuwa Julai 14, 2022 katika Ukumbi wa Holiday In – The Business Park Najma Al Masa Ball Room.

Baada ya hapo, Jumamosi ya Julai 16, 2022 atapafomu Live akiwa na DJ Seven na Dj Liya huko Dubai.


 
Ikumbukwe kuwa, mara tu baada ya kurudisha penzi lao, Harmonize alimtambulisha Kajala kama mmoja wa Mameneja wake ambaye atakuwa akifanya kazi ya kusimamia kazi zake na kazi za wasanii wengine ww Lebo ya Konde Music.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad