Kesi ya Sabaya Yapigwa Kalenda TENA Kisa Hichi HapaHakimu Mfawidhi wa Mahakama ya hakimu mkazi Moshi Salome Mshasha ameutaka upande wa Jamhuri kukamilisha upelelezi wa kesi ya uhujumi uchumi inayomkabili aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, lengai ole Sabaya na wenzake wanne.


Hatua hiyo imefuatia ombi la upande wa Jamhuri kuomba tarehe nyingine kwa madai kuwa upelelezi wa shauri hilo haujakamilka, pamoja na kutokamilika kwa hati ya kuipa mamlaka mahakama hiyo kusikiliza shauri hilo.


Hakimu Mshasha amesema ni vema upelelezi huo ukakamilika mapema ili shauri hilo lianze kusikilizwa na washtakiwa wajue hatma yao.


Awali wakili mwandamizi wa serikali Kassimu Nasri amedai mahakamani hapo kuwa, bado upelelezi wa shauri hilo haujakamilika na hivyo kuiomba mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa ili wakamilishe upelelezi pamoja na vibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini.


Kwa upande wake Wakili wa utetezi Helen Mahuna amesema hawapingani na hoja za upande wa mashtaka, lakini amedai kuwa upande wa mashtaka haulichukulii uzito shauri hilo kutokana na kuahirisha mara kwa mara.


Mbali na Ole sabaya, washtakiwa wengine ni Silivester Nyegu, John Aweyo, Nathan Msuya na Antero Assey ambao wanakabiliwa na mashtaka saba ikiwemo kuendesha genge la uhalifu, kupokea rushwa, utakatishaji wa fedha pamoja na ukiukwaji wa mamlaka ya utumishi.


Shauri hilo limeahirishwa hadi tarehe 14 mwezi huu litakapotajwa tena.

______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad