Ticker

6/recent/ticker-posts

Kilichomuua Bi Hindu, familia yafunguka
Dar es Salaam. Msanii Chuma Suleiman maarufu kama Bi Hindu amefariki dunia baada ya kuugua kansa ya mapafu kwa muda mrefu

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu, mtoto wa Bi Hindu, Mwanadini amethibitisha kifo cha mama yake.

Mwanadini amesema mama yake amefariki dunia leo Jumamosi Julai 9, 2022 akiwa nyumbani kwake Magomeni jijini Dar es salaam baada ya kuumwa kwa muda mrefu.

"Tulitoka hospitali na kumuuguzia nyumbani ambapo alikuwa anapumulia mashine ya 'Oxygen machine' kwa ufupi Watanzania wafahamu hilo, tutaendelea kuwajulisha mengine kwa kadri tutakavyoweza".amesema.


 
Mwanaidi amesema bado hawajapanga ratiba za mazishi hadi watakapokaa kikao cha ndugu kujua watazika lini na wapi.

"Kupitia nyinyi tunawaambia mashabiki wa mama yetu Bi Hindu kwamba msiba upo Magomeni mtaa wa Uweje, tutaendelea kuwapa taarifa nyingine kadri tutakavyopata maamuzi ya nini tufanye". amesema Mwanadini na kuongeza;

"Mama alikuwa na watu wengi kuanzia kwenye kazi yake ya sanaa hadi kwenye upenzi wake na Simba, hivyo naamini wakipata taarifa hii watajumika nasi".

Amesema watamkumbuka mama yao kwa upambanaji wake na kusimamia anachokiamini bila kujali Dunia inakaa kinyume naye.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments