Kimenuka..Serikali yataifisha Dawa za Binadamu Aina 34

 


Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imetaifisha aina 34 za dawa za binadamu zilizokamatwa zikiuzwa kiholela mitaani kwenye maduka ya dawa za binadamu zaidi ya mia mbili yasiyo na usajili kwa mikoa mitatu kanda ya ziwa magharibi kunusuru afya za watu.


Meneja TMDA Kanda ya Ziwa Magharibi Dkt. Edgar Mahundi, amesema wanaendelea na oparesheni hiyo duka kwa duka na dawa zilizotaifishwa zitagaiwa kwa wananchi bure.


“Zimekutwa katika haya maeneo kwanza baadhi ya maeneo hajasajiliwa kuuza aina hii ya dawa, lakini pia hizi dawa ni dawa moto wale wauzaji waliokutwa kule walikuwa hawana sifa ya kuziuza hizi dawa,” amesema Dkt Mahundi.


Naye, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita Dkt. Japhet Simeo amesema uuzwaji holela wa dawa za binadamu mitaani husababisha athari kubwa za kiafya kwa mtumiaji.


“Kuna dawa zingine zinapotumika zinaweza kuleta madahara kama ni mjamzito kiumbe kilichopo tumboni kinweza pata madhara, ndio maana tunasema lazima mtua aende akapate ushauri wa kitaalamu ili aweze kutumia dawa,” amesema.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Rosemerry Senyamule amewataka TMDA kuendelea na operashini hiyo katika maeneo yote ili kunusuru afya za watanzania.

______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad