Ticker

6/recent/ticker-posts

Kipa Manula Ampisha Mshery StarsKOCHA mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen amefanya mabadiliko kwenye eneo la kipa ambapo Aboutwalib Mshery amechukua nafasi ya Aishi Manula kwenye mchezo wa kufuzu fainali za Mataifa Afrika kwa Wachezaji wa ndani (CHAN) mwakani nchini Algeria 2023 dhidi ya Somalia.

Hatua hiyo inakuja baada ya Manula kupata majeraha kwenye mchezo wa kwanza baina ya timu hizo uliopigwa Julai 23, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Katika mchezo huo wa mkondo wa kwanza Stars iliibuka na ushindi wa bao 1-0, lililofungwa na kiungo mshambuliaji, Abdul Suleiman 'Sopu '.

Kikosi kamili kinachoanza mechi ya leo ni Aboutwalib Mshery, Mohamed Hussein 'Tshabalala', Kibwana Shomari, Dickson Job, Bakari Mwamnyeto, Mzamiru Yassin, Salum Aboubakar 'Sure Boy', Abdul Suleiman 'Sopu', Feisal Salum 'Fei Toto', George Mpole na Kibu Denis.


Stars inahitaji ushindi au sare tu kufuzu hatua inayofuata ambapo itacheza na Uganda.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments