Ticker

6/recent/ticker-posts

Kisa Bangi ya Makonda Harmonize na Sallam SK Walikaa Mwaka Mmoja Bila Kuzungumza Wala Kusalimiana


Sallam Sk ameweka wazi kuwa hakuwahi ongea na Harmonize mwaka mzima akiwa bado yupo WCB, Akifunguka kwenye kipindi cha Salama Na, Sk amedai tatizo lilianzia pale tu aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, mstaafu Makonda kutamka kuwa Harmonize anavuta bangi na inabidi aripoti central ili apimwe, ishu ambayo ilimkasirisha Harmonize na kumwambia SK kuwa Babu Tale ndiye aliye mwambia makonda mambo ya Bangi.


SK anadai kiukweli hakuna aliye mwambia Makonda kuhusu Harmonize kula bangi, na baadhi ya Viongozi waliwahi wafwata na kuwaambia kuwa WCB ni kioo cha jamii lakini tabia ya Konde boy kutafuna kijiti hadharani si nzuri, na kwakua tayari Konde alimnyooshea Tale kidole kama ndiye aliye mchoma kwa Mh. Makonda, ikabidi Sk amkingie kifua Tale kwa kujifanya kuwa yeye ndiye aliye mwambia Makonda, na hapo ndipo ukawa mwanzo na mwisho wao wa kuzungumza.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments