Ticker

6/recent/ticker-posts

Kutana na Mdau Anaeota Ndoto za Mchana Kuwa Anafanya Kazi Simba Huku Akiwa Amemuoa Wema Sepetu

 


Shabiki huyo wa klabu ya Simba anayeitwa Moud afunguka


"Mashabiki Wenzangu wa Simba Em Semeni wenyewe, Ni Raha ya kiasi gani Mimi ntakayoipata Moud Wenu Siku nikipata kazi hata yakubeba mabegi ya wachezaji tu pale Simba ,,,,Em Semeni wenyewe "wachezaji wenye hadhi wanaotambulika Hadi Kwenye Tuzo za CAF Kuna ubaya Mimi nikiwa nawabebea mizigo Yao ?


Bila ya Shaka Hakuna ubaya Kuna kila sababu ya Raha pale msimbazi, Imagine ndio nakubaliwa lile ombi langu Halafu ndio unabeba Mkoba Wa Pape Sakho Ndani Yake kukiwa Na Kiatu Cha dhahabu ' Raha iliyoje,,,


Hivi mshaelewa kwanini nawaombaga kazi Simba kila siku na huu mwaka wa 5? 🤪, Nadhani majibu juzi mliyapata hakuna mtu asiyependa kufanya kazi sehemu ambayo Kuna mafanikio makubwa, Hakuna mtu asiyependa kufanya kazi sehemu ambayo ataandika japo historia yakupiga tu picha na kiatu Kama Cha Sakho 🤪


Okay, Nafikiri majibu mmeyapata juzi,,,,


Sasa Vuta picha ndio nimepata kazi Simba halafu Madame Wema Sepetu ndio kanikubalia ombi langu ili nimuowe Ni Raha kiasi gani ntakayoipata Mimi Jamani Moud wenu,,,


Yaani itakuwa natoka Nyumbani naenda kuhudumu kwenye club kubwa Africa mashariki na Kati (Simba) Halafu nikirudi home Nakuta mahaba ya Madame Wema 🥰,,,,Vuta picha mwenye hapo uone Raha ntakazopata Mimi Moud wenu,,,


Bila ya shaka itakuwa Kama nipo Pepon Raha za Simba Jumlisha na Mahaba ya mtoto mzuri Kama Wema Sepetu Najihisi Nitakuwa Dunia ya pekeangu Mshikaji wenu Mimi Niombeeni Nikubaliwe kazi Kule Simba hata yakutunza uwanja tu Kisha mniombee Tena Kwa Wema Sepetu anikubalie Ombi langu nipo seriously Nataka nimuoe ndani ya mwaka huu tu Kama atakubali. NARUDIA TENA NIPO SERIOUSLY

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments