Ticker

6/recent/ticker-posts

Machozi ya Issa Azam Kisa Mange Kimambi Yanakamilisha Usemi Kuwa Malipo na Hapa Hapa Duniani


Sina maana kuwa lisemwalo lipo na wala sina hakika na hilo, ila najaribu kuyawaza maumivu anayo yapitia @issaazam kwa hivi sasa hadi kutokwa machozi kwenye interviews. Kilio cha Issa Azam kinatokana na kusemwa, mdomo anao utumia kulalamika kusingiziwa skendo yake, ndio huo huo anao utumia kuwakejeli na kuwaongelea maneno ya shombo watu wengine.

Harmonize na Alikiba ni miongoni mwa wasanii walio pakazwa vibaya na huyu jamaa, na Sasa hivi kahamia kwa Rayvanny. Ana undugu na Kiba, lakini namna alivyo msema kwenye moja ya interview, sidhani kama Ali ana hamu naye tena, yote haya akiyafanya kutaka kuwa karibu na Diamond (uchawa).

Harmonize angekuwa anaenda kwenye interview na kulalamika anavyo semwa na huyu jamaa, sijui ingekuaje.


Masuala ya mimi nina Mama tu, ananitegemea, nadhani angeanza kufikiria wazazi wa wenzie kwanza wanapokeaje kejeli anazo zitoa kwa watoto wao. Malipo ni duniani, iwe kweli isiwe kweli, Mungu anakupa mtihani wa kupita kwenye maumivu, wanayo pitia wengine ukiwa wewe ndiye msababishaji.


Pole sana Issa, ila Kumbuka maisha gwaride, Ukisikia nyuma geuka.....

Sajo

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments