Ticker

6/recent/ticker-posts

Manara: Naliona kombe la Afrika Yanga 
MSEMAJI wa klabu ya Yanga, Haji Manara amesema Uongozi utakaochaguliwa leo anaona kabisa Yanga ikichukua kombe la Afrika miaka mitatu mbele.
MSEMAJI wa klabu ya Yanga, Haji Manara amesema Uongozi utakaochaguliwa leo anaona kabisa Yanga ikichukua kombe la Afrika miaka mitatu mbele.

Manara ameyasema hayo leo kabla ya mkutano wa uchaguzi wa klabu hiyo kufunguliwa rasmi  na Mtendaji mkuu wa klabu hiyo, Senzo Mbatha.
Akizungumza mbele ya Wajumbe wa Mkutano mkuu, Manara amesema akiwa sehemu ya Sekretarieti ya timu hiyo anaona viongozi wanaochaguliwa leo wataifikisha timu hiyo mbali.

“Nyie ambao mpo hapa wanachama wanawategemea muwachagulie viongozi wa kuipeleka Yanga mbele,” amesema Manara na kuongeza;

“Nyie ambao leo mpo hapa tunataka muwepo kwenye rekodi ya timu yetu kwamba mmechagua mabadiliko mapya kwenye timu.”

Baada ya kuyasema hayo, saa 6:17 Senzo alifungua mkutano wa uchaguzi na kusema ajenda kubwa ni uchaguzi.

“Sina maneno mengi leo kabisa, ajenda yetu ni uchaguzi na hiyo ndio itaendelea hapa, amesema Senzo.


Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments