Mchezaji Aliyewatungua Yanga Matatu Fainali ya Kombe la Azam Ala Shavu Nono Azam FC


Uongozi wa klabu ya Azam FC, umemtangaza Abdul Seleman (Sopu), mchezaji wao mpya baada ya kumsainisha mkataba wa miaka mitatu.


Mchezaji huyo ambaye aliwahi kupita katika klabu ya Simba, ameonesha kiwango cha hali ya juu msimu huu akiwa na klabu ya Coastal Union.


Mwishoni mwa wiki iliopita, mchezaji huyo akiitumikia Coastal Union, alifanikiwa kufunga mabao matatu pake yake kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la FA dhidi ya Yanga huku ukimalizika kwa sare ya mabao 3-3 kabla ya Yanga kuibuka na ushindi kwa mikwaju ya penalti.


Hata hivyo, Sopu kabla ya kujiunga na Azam FC alikuwa anahusishwa kutua Yanga SC au kurudi Simba, lakini Azam wameonesha ubabe wao.


Azam FC msimu ujao unadhani itakuwa ya aina gani?

______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad