Injinia Hersi Said "Tutaweka Rekodi ya Yanga kuwa timu ya kwanza kubeba ubingwa wa Caf"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPAMGOMBEA wa Urais wa Yanga ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya klabu hiyo, Injinia Hersi Said, ametoa ahadi ya kuweka rekodi ya kuifanya Yanga kuwa timu ya kwanza kubeba ubingwa wa Caf.

 

Kauli hiyo aliitoa juzi katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi huo utakaofanyika kesho Jumamosi katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Posta jijini Dar es Salaam.

 

Yanga ambayo imebeba mataji matatu – Ligi Kuu Bara, Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) na Ngao ya Jamii, inatarajiwa kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Hersi alisema kuwa anataka kuona ndani ya kipindi cha uongozi wake analeta Kombe la Caf.

 

Hersi alisema kuwa hilo linawezekana kwake kutokana na mikakati atakayoiweka ikiwemo kusuka kikosi imara cha wachezaji bora wa kiwango kizuri aliongeza kuwa kikubwa wanachama wampe dhamana ya kuiongoza timu hiyo, kwa kumpa Urais.

 

“Ninataka kuona timu yetu ya Yanga inaweka rekodi ya kwanza ya kubeba ubingwa wa Afrika na hilo linawezekana kwetu “Ahadi hiyo ninaitoa kama siyo msimu huu au ujao kutokana na mikakati niliyoiweka kama nikiwa Rais wa Yanga.

 

“Nafahamu hivi sasa kila timu itaiangalia Yanga kimataifa kutokana na usajili ambao tumeufanya wa kutikisa Afrika, tukiwa tumetoka kuwatangaza wachezaji wetu wawili, Morrison (Bernard) na Kambole (Lazarous),” alisema Hersi.

Stori: Wilbert Molandi
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad