Mke aenda kudai talaka akiwa na hawara, wapigwa risasi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPAMwanamume mmoja (61) amemuuwa kwa risasi mpenzi wa mke wake (44), kufuatia majibizano wakati mkewe huyo (28) alipopandisha hasira akidai talaka katika eneo la Houston kaskazini, nchini Marekani.

Afisa wa masuala ya usalama wa eneo hilo, Sheriff Ed Gonzalez amesema kisa hicho kilitokea katika mgahawa wa Crab Station, ulioko 4505 FM 1960 majira ya saa sita mchana n akudai kuwa mtu yeyote mwenye undani wa tukio hilo anaombwa kuwasiliana na Kitengo cha Mauaji kwa simu namba 713-274-9100.

Amesema, wawakilishi wa Ofisi ya Sheriff wa Kaunti ya Harris walisema mwanamume huyo alikuwa akikutana na mke wake kwa ajili ya maongezi juu ya talaka lakini mkewe alifika katika eneo la makubaliano akiwa na ameambatana na mpenzi wake mpya.


Nje ya eneo la tukio katika mkawawa uliopo Kaunti ya Harris (Picha kwa hisani ya mtandao wa Bksfe)
“Wakiwa katika eneo hili kulitokea mabishano ambayo yalichaginzwa na mpenzi mpya kitu ambachi kinaonesha hakukipenda na alishindwa kudhibiti hasira zake akafanya mauaji ya risasi na ndipo tukatoa taarifa,” amesema Gonzalez.


 
Wanasema mwanaume huyo aliwasili na maongezi yao yalidumu kwa dakika 20, kabla ya kuinuka na kwenda katika gari lake aina ya Maserati yenye rangi nyeusi nyeusi na kuchukua Bunduki mbili.

“Alimpiga risasi mpenzi wa mke wake na kumuua kisha alijaribu kumpiga risasi mke wake lakini akakosa na baadaye Wafanyakazi walipiga simu 911 wakati mtuhumiwa akiondoka eneo la tukio na gari lake Maserati nyeusi,” amefafanua Afisa huyo wa Polisi.


Gari aina ya Maserati aliyokuwa akiitumia mshukiwa siku ya tukio (Picha kwa hisani ya mtandao wa Bksfe)
Hata hivyo, inadaiwa kuwa baada ya kufanya tukio hilo na kuondoka Polisi walimfuatilia na kumpata umbali wa yadi 100 akiwa katika eneo la maegesho ya barabara, na walipokaribia alishuka kwenye gari na kujipiga risasi kichwani.


Mshukiwa huyo, alipelekwa katika hospitali ya eneo hilo akiwa na hali mbaya na Polisi haijafafanua kuhusu hali yake ingawa imesema bado uchunguzi wa tukio hilo unafanywa na Kitengo cha Mauaji cha Ofisi ya Sheriff Kaunti ya Harris.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad