Ticker

6/recent/ticker-posts

Muongozaji Mkongwe wa VIDEO Tanzania Adam Juma Aibuka na Kumtetea P Funk Ugomvi na Salam SK "Heshima Ibaki"


Muongozaji mkongwe wa video nchini, Adam Juma amesema heshima ya Producer P Funk Majani ibaki pale pale.

"Huyu mzee tuseme yote heshima yake kwenye tasnia yetu ibaki pale pale vinginevyo dunia itakua nyeusi sana. Hatuna nguvu ila tupo wengi. Vita ya mawe kwenye kokoto" - Ameandika Adam Juma  kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Adam ameeleza hayo kufuatia kuwepo kwa mkanganyiko wa taarifa, ambapo kwenye mahojiano ya P Funk na bongo5, akijibu swali la mtangazji Yasin kuhusiana na madai ya wasanii na lebo zao akitolea mfano wa lebo ya WCB, P Funk alijibu swali hilo akisema, mfumo unaotumika na lebo ya WCB kusimamia wasanii sio mfumo rafiki kwani wanadidimiza msanii kwa kuchukua asilimia kubwa na msanii anabaki na ndogo.

Kauli hiyo ya Majani ilipokelewa tofauti kwa upande wa WCB na kupelekea kuwepo kwa majibizano mtandaoni yaliyoanzishwa na Baba Levo kisha baadae meneja wa msanii Diamond Platnumz, Sallam SK ambaye nae alitoa neno lake kuhusiana na hilo.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments