Mwanafunzi ajifungua chumba cha mtihani Simiyu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





Maswa. Mwanafunzi wa darasa la saba, Shule ya Msingi, Kulimi, Kata ya Kulimi wilayani Maswa, Mkoa wa Simiyu amejifungua katika chumba cha mtihani Julai 27, 2022.

Taarifa iliyotolewa na ofisa elimu Mkoa huo, Majuto Njaga ameiambia Mwananchi Digital tukio hilo lilitokea Julai 27, 2022 wakati mwanafunzi huyo akiwa katika chumba cha mtihani.

Amesema idara ya elimu wilayani Maswa ilitoa taarifa katika ofisi yake na kueleza kwa kipindi chote cha ujauzito walimu hawakuwa wanafahamu kama mwanafunzi huyo ni mjamzito.

"Alijifungua akiwa shuleni, baada ya kujifungua ofisi ya elimu kwa kushirikiana na maafisa wa ustawi wa jamii walifika shuleni hapo na binti alimtaja aliyempa ujauzito na tayari kesi imefunguliwa," amesema Majuto.


 
Amesema baada ya maafisa wa ustawi wa jamii kufika shuleni hapo, mtoto alikabidhiwa kwa wazazi wake akiwa na mwanaye kwa ajili ya uangalizi zaidi.

Aidha, amesema baba wa mtoto aliyetajwa ni mkazi wa maeneo hayo na sio mwalimu.

Akijibu hatma ya elimu ya mtoto aliyejifungua, Njanga amesema kwa mujibu wa waraka wa elimu uliopo, ataruhusiwa kurudi shule kwa kurudia darasa alilokuwepo awali baada ya mwaka mmoja ikiwa ni takwa la kumpa haki mtoto kunyonyoa maziwa ya mama kwa kipindi hicho.


Kaa karibu na Mwananchi Digital kwa taarifa zaidi juu ya tukio hili.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad