Ticker

6/recent/ticker-posts

Mwili wa Mkufunzi wa Sensa Aliyefia ‘Gesti’ Wazikwa
Tabora. Mwili wa aliyekuwa mkufunzi wa sensa ya watu na makazi 2022, Bahati Msengi (47) aliyefariki dunia katika nyumba ya kulala umezikwa leo Jumamosi, Julai 30, 2022 mjini Tabora.

Msengi alikutwa amefariki dunia Jumatano Julai 27, 2022 saa nane mchana katika nyumba ya kulala wageni ya Wema, Tabora mjini.

Mkufunzi huyo ambaye pia alikuwa afisa elimu kata ya Milambo, wilayani Kaliua mkoani humo, alihudhuria mafunzo ya siku 21 yaliyomalizika siku moja kabla ya kufikwa na mauti.

Mmoja wa walimu waliomfundisha mkufunzi huyo ambaye alikuwa afisa elimu kata, tarafa ya Ulyankulu, wilayani Kaliua, Musa Kabimba amesema walikuwa wanalala nyumba hiyo pamoja kwa siku zote za mafunzo.


Amesema mchana siku ya kufunga mafunzo alielezwa na Msengi anajisikia kuumwa na kuomba ruhusa

Kalimba amesema kwa vile walikuwa wanatoka usiku, siku ya mwisho alilala hadi saa tano alipogongewa na mhudumu wa sehemu hiyo kueleza amechoka anataka kuendelea kupumzika.

"Mhudumu aliponigongea nilimueleza nimechoka na kweli nilikuwa nimechoka na kumweleza sitaki kufanyiwa usafi siku hiyo," amesema


Amesema baadae alifika mwendesha bodaboda saa sita au saba mchana akimuulizia mkufunzi huyo na kuelezwa na mhudumu amepumzika kwani atakuwa amechoka kama mwenzake akimaanisha yeye.

Hata alipopigiwa simu bado ilikuwa haipatikani na ndipo walipozunguka dirishani na kumuona amelala na simu ipo pembeni.

"Yule mwendesha bodaboda alieleza kwamba mwenzetu atakuwa amefariki na mhudumu kumshika mkono na baadae vidole na kubaini kweli amefariki," amesema

Juzi, Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema tukio hilo ni kifo cha kawaida kama vifo vingine vinavyotokea hospitalini.


Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments