Ticker

6/recent/ticker-posts

Mwimbaji Tems Alamba Dili Nono...Sauti yake Akiimba Kusikika Kwenye Movie Mpya ya Blank Panther Wakanda Forever


Mwimbaji hodari wa Kike toka nchini Nigeria TEMS (@temsbaby) ameendelea kukesha kwenye headlines za dunia, leo ameibuka na hii ya kushirikishwa kwenye Soundtrack ya filamu ya “Black Panther: Wakanda Forever” ambayo itatoka rasmi November 11, 2022.

Sauti ya Tems inasikika mwanzoni kabisa mwa trailer ya filamu hiyo, akiimba wimbo wa Bob Marley “No Woman, No Cry” kwenye moja ya mahojiano yake na Billboard, Tems aliwahi kuutaja wimbo huo wa hayati Bob Marley kama miongoni mwa nyimbo zake pendwa.

Hili ni shavu lingine kubwa kumuangukia Tems ndani ya wiki moja, wiki hii pia ametajwa kuwa miongoni mwa waandishi walioshiriki kuandika nyimbo kwenye Album ijayo ya Beyonce “Renaissance” akiandika wimbo uitwao “Move”

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments