Ticker

6/recent/ticker-posts

P Funk Majani: Paula Atabadilika Tabia, Sasa Naongea Naye Vizuri

Nafasi za Ajira Serikalini Zilizotangazwa Wiki Hii Bonyeza HAPA

Nafasi za Internship Zilizotangazwa Bonyeza HAPA

Matokeo ya Form Four 2022 Bonyeza HAPA
Paula ni mtoto wa P Funk Majani pamoja na Kajala Masanja
PRODYUZA mkongwe wa muziki Bongo, P Funk ‘Majani’ amesema kuwa, mwanaye Paula anayo nafasi kubwa ya kubadilika tabia kwani sasa ameanza kujitambua na kuwa mtu mzima.

Majani amesema hayo hivi karibuni wakati akifanyiwa mahojaiano na vyombo vya habari huku akisema kuwa kwa sasa anaongea vizuri na mwanaye huyo huku akimsihi kuendelea kufanya vitu anavyovipenda ili afanikiwe katika maisha yake sambamba na kumtakia heri ya siku ya kuzaliwa.

“Nachomtakia Paula awe independent (ajitegemee) kwenye fikra zake na aanze kutafuta maisha yake kwa mfumo wake anaoutaka yeye. Afuate moyo wake na afanye kitu anachokipenda na awe na passion. Ukifanya kazi unayoipenda utafanikiwa lakini usifanye kazi ambazo ni angalau, unavamia fani, utapotea.

“Aliniambia anazindua duka lake la mavazi, namtakia kila la kheri na nipo kwa ajili yake, kumshauri. Siku hizi tunaongea vizuri sana, tunaenda vizuri na ameanza kuwa mtu mzima sasa.


Paula mtoto wa Kajala na Majani
“Mimi sio mpenzi mkubwa wa masuala ya mitandao kwa watoto wangu, hata mara ya kwanza sikupenda lakini ilikuwa ngumu kuzuia kwa sababu anaishi kwa mama yake mzazi. Yale yameshapita na yeye ameshajua namna ya ku-controil mitandao, mitandao ishamcharaza mara kibao na sasa anajua namna ya kumudu mtandao kwa ajili ya kujenga brand yake.

“Lakini kuna wajinga wachache watakutukana wataandika hiki ili kukuchafua, ukishawazoea haikusumbui kitu. Mimi naona ni wajinga tu, ukikaa ukaona mtu anaandika ujinga unasema huyu ni mpumbavu tu. Ukibishana nao unajishusha na unakuwa mpuuzi na wewe,” amesema Majani.

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Tanzania Zipo HAPA

Ufadhili wa Masomo ( Scholaships) Bonyeza HAPA

Post a Comment

0 Comments