Rais Samia Aelekeza Kujengwa kwa Mnara wa Makao Makuu ya Nchi Jijini Dodoma

 


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa maagizo kwa Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kutafuta eneo kubwa na zuri kwa ajili ya ujenzi wa Mnara wa Makao Makuu ya nchi jijini Dodoma.


Rais Samia ameyasema hay oleo Julai 25, 2022 katika maadhimisho ya siku ya Mashujaa ambayo yamefanyika Kitaifa mkoani Dodoma.


“Kutokana na umuhimu wa siku hii nataka kupendekeza kwamba kwa kuwa Jiji la Dodoma linakua na Uwanja huu tupo katikati ya Mji nipendekeze kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu Ofisi yako pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kutafuta eneo kubwa na bora zaidi kujenga Mnara wenye hadhi ya Makao Makuu ya Nchi kwa gharama zitakazo sitahimilika.” Amesema Rais Samia.


Aidha Rais Samia ametoa pongezi za dhati kwa waasisi wa Taifa la Tanzania akiwemo Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume kwa mchango na ushujaa wao katika maendeleo ya Taifa la Tanzania.


Wananchi wamejitokeza kwa wingi katika maadhimisho ya Siku ya Mashujaa yaliyofanyika Kitaifa Jijini Dodoma


Mbali na Rais Samia Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili Ali Hassan Mwinyi, Rais wa Awamu ya Nne Dkt, Jakaya Mrisho Kikwete, Mawaziri Wakuu John Malecela, Frederick Sumaye pamoja na Mizengo Pinda.


Kwa upande mwingine Rais Samia ametoa rai kwa wananchi kuendelea kudumisha Amani na upendo kwani kwa kufanya hivyo ni kuendeleza tunu na kazi iliyofanywa na waasisi wa Taifa la Tanzania.

______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad