Ticker

6/recent/ticker-posts

Rayvanny "Ucheleweshaji wa Baadhi ya Mambo na Asilimia za Mkataba ni Sababu ya Rayvanny Kuondoka WCB"


Professional Chawa wa Diamond Platnumz na Mtagazaji wa kipindi cha MGAHAWA cha Wasafi Fm, @officialbabalevo ametaja baadhi ya sababu zilizo pelekea @rayvanny kuondoka WCB.

Akifunguka mbele ya waandishi wa habari kwenye viunga vya Mlimani City kama mmoja wa wahudhuriaji wa harusi ya Billnas pamoja na Nandy iliyo fanyika usiku wa kuamkia leo Tarehe 16/17 July, Baba Levo amedai hoja kubwa alizotoa Rayvanny na yeye kama Baba Levo akaona zina mashiko ni suala la asilimia (mikataba) na ucheleweshwaji wa baadhi ya vitu (ambavyo hakuviweka hadharani).

Mbali na hilo Baba Levo amedai yote haya Diamond anayajua, na ametengeneza mikataba ambayo siku msanii akiamua kuindoka lazima aache pesa mezani kwasababu, wasanii wanatamani kuwa karibu na Diamond ili wawe wakubwa, na wakishakuwa wakubwa wanaona kukaa karibu na Diamond wanaonekana wadogo, so lazima kuwe na mikataba konki hata siku msanii akiamua kuondoka, kuwe na uhalali wa pande zote mbili (Lebo na msanii)

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments