google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Serikali kukutana na Tucta kutoa ufafanuzi nyongeza ya mishahara | UDAKU SPECIAL

Serikali kukutana na Tucta kutoa ufafanuzi nyongeza ya mishahara

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Dodoma. Serikali ya Tanzania Jumatatu Julai 26, 2022 itakutana na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) ili kuwasikiliza na kutoa ufafanuzi kuhusu nyongeza ya mishahara Julai mwaka huu.


Taarifa hiyo imetolewa leo Jumapili, Julai 24, 2022 na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa katika ukarasa wake wa mtandao wa Twitter.


“Ndugu wafanyakazi, Jummane tarehe 26 Julai 2022 Serikali itakutana na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) ili kuwasikiliza na kutoa ufafanuzi kuhusu nyongeza ya mishahara katika mishahara ya Julai 2022,”amesema.


Mei 14, 2022, Rais Samia Suluhu Hassan aliridhia mapendekezo ya kuongeza mishahara ikiwemo kima cha chini kwa watumishi wa umma kwa asilimia 23.3 ambayo yangeaza katika mshahara wa mwezi Julai.


Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus ilisema mapendekezo hayo ni mwendelezo wa kikao cha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alichokifanya mkoani Dodoma na kupokea taarifa kutoka kwa wataalamu kuhusu ongezeko la mishahara.


Taarifa hiyo ilisema Serikali imepanga kutumia kiasi cha Sh9.7 trilioni katika mwaka wa fedha 2022/23 kwa ajili ya kugharamia malipo ya mishara ya watumishi wote katika Serikali Kuu, Serikali za Mitaa, Taasisi na Wakala za Serikali.


Nyongeza hiyo ilikuja siku chache baada ya Rais Samia kuwahakikishia wafanyakazi nchini kuwa Serikali katika mwaka wa fedha 2022/2023 itaongeza mishahara kwa watumishi wake.


 Rais Samia alitoa ahadi hiyo Jumapili Mei Mosi 2022 wakati wa sherehe za wafanyakazi duniani zinazofanyika katika uwanja wa Jamuhuri jijini Dodoma.


Taarifa hiyo imekuja siku moja baada ya Msigwa kuwaomba wafanyakazi watulie, Serikali itatoa ufafanuzi kuhusu nyongeza ya mishahara hiyo.



-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad