Ticker

6/recent/ticker-posts

Sheikh Mkuu Dar amuombea Majaliwa aongeze mke wa piliSHEIKH Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum amemuombea Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aoe mke wa pili ilia pate utulivu zaidi katika mizunguko yake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Sheikh Alhad ametoa kauli hiyo leo tarehe 2 Julai, 2022 wakati akisoma dua katika kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya duniani yanayofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Kauli hiyo iliwaacha hoi washiriki wa maadhimisho hayo akiwamo Waziri mkuu ambaye sasa ameoa mke mmoja anayefahamika kwa jina la Marry Majaliwa.

Katika maombi hayo Sheikh Alhad ameomba hivi; “Tunamuombea sana Waziri mkuu ambaye ndiye mgeni rasmi wa jambo hili, tumeshuhudia hasa sisi viongozi wa dini namna ambavyo na akijituma kwa ajili ya watanzania.


“Suala la sana suala la Ngorongoro, Loliondo… Waziri mkuu ammewathibitishia Watanzania kwamba serikali ina nia njema na raia wake na hakuna raia ambaye atakosa haki au kunyanyaswa kwa namna yoyote ile, amekuwa halali hapumziki.

“Tunamuombea Mwenyezi Mungu aendelee kumbariki Majaliwa Kassim Majaliwa na ikikupendeza aongeze pia mke wa pili aweze kupata utulivu zaidi katika mizunguko yake,” ameomba Sheikh huyo.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments