Simba yapokea kichapo Misri, Phiri aumiaLABU ya Simba imepoteza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Haras El Hodoud ambao wamepanda daraja kucheza Ligi Kuu nchini Misri msimu ujao.

Mabao ya El Hadoud yalifungwa dakika ya pili kwa mkwaju wa penalti na Mahmoud Guda huku la pili likiwekwa kimiani na Mahmoud Mamduh dakika 10 baada ya kipindi cha pili.

Katika mchezo huo mshambuliaji wa Simba, Moses Phiri alishindwa kuendelea na mechi dakika ya 41 baada ya kupata maumivu makali huku nafasi yake ikachukuliwa na kiungo Victor Akpan.

Mchezo huu ni wa tatu wa kujipima nguvu kwa miamba hiyo ya kocha Zoran ambaye anaendelea kukinoa kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao.


Katika michezo miwili iliyopita Simba ilianza kwa kufungana bao 1-1 na Ismailia kabla ya kushinda mabao 6-0 dhidi ya Abo Hamad.

Baada ya mchezo huo kumalizika, ofisa habari na mawasiliano wa klabu hiyo Ahmed Ally kupitia kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram aliandika;

"Kupoteza kwenye kujifunza, kupoteza kujenga timu na kupoteza kwenye manufaaa,"
______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad