Ticker

6/recent/ticker-posts

Steve Nyerere Achimba Mkwara Harusi ya Nandy na Billnass, Aahidi Kufanya Kufuru

Steve Nyerere ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Harusi ya Billnass na Nandy
IKIWA ni siku mojaa baada ya kuchaguliwa kwa msanii maarufu nchini, Steve Nyerere ibu ya kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Harusi ya wasanii wenzake, Billnas na Nandy, hatimaye Steve asiyeishiwa vituko amekuja na jipya.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Steve amewashukuru Billnas na Nandy kwa kumpa heshima hiyo ya uenyekiti huku akiahidi kusimamia harusi hiyo na kuwa ya viwango vya juu.

”Billnas na Nandy nichukue nafasi hii kusema asanteni sana, nimekaa nimelitafakari ombi lenu nimelichambua kwa kina nikasema ya nini nikatae, ndoa ni jambo kubwa na baraka pia.


Billnass na Nandy wanatarajiwa kuoana hivi karibuni
“Niseme tu hiii sio harusi, ni wedding watu wengi wanafanya harusi, sisi tunaenda kufanya wedding. Ni wedding ambayo toka uhuru wa taifa hili haijawahi kutokea.


 
“Nyie hamuendi kufanya harusi mnafanya wedding chini ya usimamizi wangu, asanteni sana. Niwape onyo wazamiaji, wedding day hatukagui kadi tunakaribisha watu na Watanzania,” amesema Steve.


Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments