Ticker

6/recent/ticker-posts

Steve Nyerere Ateuliwa Kuwa Mwenyekiti Harusi ya Nandy na Billnass Afunguka Haya


Baada ya muda mfupi tu hii leo, Msemaji mstaafu wa shirikisho la muziki nchini, @stevenyerere2 kulamba teuzi la uwenyekiti wa harusi ya @billnass na @officialnandy , amedai amepata simu nyingi za pongezi kutoka sehemu mbalimbali duniani, Simu kutoka Ujerumani, South Africa, Mtwara, Tanga na maeneo mengine hadi simu ikazima.

Akibonga na @soudybrown kwenye U-HEARD, Tivu akee ayiii amedai kapewa heshima kubwa sana kuteuliwa kwenye nafasi hiyo, na anaenda kufanya jambo kubwa sana, toka nchi ipate uhuru basi hii itakuwa harusi ya kipekee sana, na sio Harusi bali wedding, mzamiaji akikamatwa hatoki nje bila kulewa, vituo mbalimbali vya habari vitaonyesha.

Lakini pia Mwenyekiti amezungumzia experience yake kwenye ishu kama hizi ambapo amedai aliwahi kuwa M/kiti kwenye Harusi ya Manara na nyingine nyingi, lakini pia amewahi hudhuria harusi ya mtoto wa malkia wa uingereza, Princess Dianna mwaka 1994😂.

Mwenyekiti kaupiga mwingi tayari😀

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments