Ticker

6/recent/ticker-posts

Tanasha Dona Amwagia Sifa Diamond Platnumz Malezi ya Mtoto Wao Naseeb Junior


Mwezi June mwaka huu, msanii Diamond Platnumz alimtembelea mwanaye Naseeb Junior huko Kenya wakati mzazi mwenzie Mwanamuziki na mrembo tokea +254, @tanashadonna akiwa yupo Ulaya, kitu ambacho kilileta furaha kwa mashabiki kuona Diamond amekuwa ni mtu ambaye yupo karibu na watoto wake tofauti na ilivyo kuwa ikionekana awali.


Baada ya tukio hilo, Mwanadada Tanasha Donna ye ameappreciate kitendo hicho cha mzazi mwenzie na kudai, Hit maker huyo wa Jeje anajaribu kuwa baba bora kwa mwanae, akibonga na Kiss Fm, Tanasha amedai...


“kiukweli si vibaya, namaanisha anajaribu kuwa baba bora kwa mwanae, napaswa kumpongeza kwa hilo.” kingine Tanasha amedai kuwa Single Mother si jambo rahisi, unazongwa na vitu vingi, kufanya kazi na kulea kwa wakati mmoja, hata kama mna mawasiliano na mzazi mwenzio, ni tofauti kama angekuwepo kabisa.


Tanasha pia ambaye ametimiza miaka 27 hivi karibu, amedai ndoto yake ni kuhakikisha anatengeneza pesa ndefu sana kabla ya kugusa miaka 30.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments