Ticker

6/recent/ticker-posts

Unataka Kupata UBUNGE Mwaka 2025, Basi Fuata Haya Ndugu Yangu Hakuna Uchawi

 

Acha kulala jiandae kuanzia sasa. Shiriki shughuli za kijamii hasa mambo kama ya misiba, ukiweza fanya harambee kwa ajili ya mfuko wa maendeleo.


Tembelea wafanyabiashara wadogo na wakubwa wa masokoni, ongea sana na vijana wenye shughuli za kila siku kama bodaboda.


Zingatia katika maongezi kuonesha utofauti wako wa kiakili na wao, zingatia mavazi yako na lugha mbele ya jamii.


Jifunze kutatua kwa mawazo au kwa vitendo penye kila mkwamo.


Jenga ukaribu na heshima kwa viongozi wa kiroho wa dini zote, shiriki kwenye vikao ambavyo vinahusu jamii inayokuzunguka, kote huko toa mawazo chanya ambayo yatatatua changomoto zao.


Uwe mtu ambaye uwepo wako unaleta nafuu kwao bila hata kutoa pesa.


NB:

Heshimu watu wote, badili nyendo zako kama uzinzi na ulevi, bila kuishi namna hii majimbo ya 2025 utayasikia mitandaoni tu.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments