Ticker

6/recent/ticker-posts

Waajiri Waogopa Kumwajiri Jamaa Huyu Wakihofia Kuwa ni Mtoto Kumbe Kala Chumvi za Kutosha


Jamaa huyo wa Kichina kwa jina la Mao Sheng(27) ameibuka kulalamikia muonekano wake huo kumponza kwa kuwa ngumu kupata kazi waajiri wakidhani ni mtoto mdogo bado


Amesema waajiri wanaogopa kumuajiri wakihofia sheria za kudhibiti ajira kwa watoto zitawachukulia hatua hivyo kuwa ngumu kwake kuendesha maisha kwa kukosa kazi licha ya kuwa mtu mzima wa miaka 27


Amesema hata hivi karibuni walienda kutafuta kazi sehemu nyingine mwenzake akapata kazi haraka lakini kama kawaida yeye akaishia kuula wa chuya waajiri wakidhani ni mtoto


Baada ya video yake kusambaa, baadhi ya waajiri wakiwemo toka Jimbo la Guangdong anakoishi wameonesha nia ya kutaka kumuajiri na updates zinasema tayari amekubali kazi mojawapo alizopewa

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments