Ticker

6/recent/ticker-posts

Wenye Silaha Wavamia Jela, Waachia Wafungwa
Abuja, Nigeria. Watu wenye silaha wametumia vilipuzi kulipua gereza karibu na mji mkuu wa Nigeria na kuwaachia mamia ya wafungwa lakini wakuu wa magereza wamesema wamewakamata tena wengi waliotoroka.

Wakazi katika eneo hilo waliripoti kusikia milipuko na milio ya risasi Jumanne jioni karibu na Kituo cha Ulinzi cha Kuje, nje kidogo ya Abuja, na vikosi vya usalama vilikuwa vimelizingira eneo hilo mapema jana.

Ofisa mmoja wa usalama aliuawa wakati watu hao wenye silaha walipovunja gereza hilo kwa kutumia vilipuzi, msemaji wa idara ya marekebisho ya tabia za wafungwa, Abubakar Umar, alisema.

“Baadhi ya wanaume waliokuwa kizuizini walitoroka. Tuliweza kuwakamata wengi wao asubuhi ya leo. Zaidi ya 300 walitoroka, lakini tumewakamata tena karibu 300,” aliwaambia waandishi wa habari jana.


Alisema maofisa wa magereza bado wanang’amua ni wangapi ambao hawajapatikana.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments