Ticker

6/recent/ticker-posts

Yanga "Tumechukua Tena Kombe"


ARUSHA. TUMECHUKUA tena hii kaui ambayo imesikia kutoka kwa mashabiki wa Yanga baada ya timu hiyo kuifunga Coastal Union 4-1 kwenye penati na kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho Azam (ASFC) 2021/22.

Yanga imetumia Coastal Union kutangaza ubingwa wa pili msimu huu baada ya kufanya hivyo Juni 15 kwenye uwanja wa Mkapa Dar na kutangaza ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2021/22.

Ushindi huo inaifanya timu hiyo kukusanya vikombe viwili msimu huu lakini pia wakitoa nafasi kwa Geita Gold kwenda kimataifa msimu ujao huku Coastal sasa ikibidi kujipanga kwa msimu ujao.

Katika mchezo huo wa fainali uliochezwa kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kipindi cha kwanza kilianza kwa kasi timu zote zikishambualiana kwa zamu ambapo Coastal ndio walikuwa wa kwanza kupata bao mapema dakika ya 11 kupitia Abdul Sopu ambaye alimalizia krosi ya Vicent Aboubakar.

Baada ya Coastal kupata bao hilo Yanga walifanya mashambulizi kadhaa ya hatari lakini kukosa umakini kwa safu yake ya ushambuliaji iliifanya dakika 45 za kipindi cha kwanza kukamilika Coastal wakiongoza 1-0.

Kipindi cha pili kocha wa Yanga alifanya mabadiliko mapema dakika ya 46 kwa kumtoa Chico Ushindi na kumwingiza Heritier Makambo kwa ajili ya kumpa Mayele usaidizi kwenye safu ya ushambuaji.

Mabadiliko hayo yalionekana kuzaa matunda kwani dakika ya 57 Yanga ilisawazisha kupitia Feisal Salum ambaye aliunganisha krosi ya Heritier Makambo.

Licha ya kurejesha bao lakini safu ya ushambuliaji wa Yanga ilikosa nafasi nyingi za wazi kupitia kwa Feisal Salum, Heritier Makambo na Fiston Mayele ambao walishindwa kukwamisha wavuni nafasi kadhaa ambazo walipata.
Dakika ya 81, Heritier Makambo aliwanyua mashabiki wa Yanga baada ya kufunga bao la pili ambalo lilidumu kwa dakika 7 kabla ya kusawazishwa na Abdul Sopu dakika ya 88 na kufanya mizani kuwa sawa.

Dakika 30 za nyongeza timu zote zilishambuliana kwa zamu ambapo Coastal walipata bao la tatu kupitia Abdul Sopu dakika ya 98 ambaye alikuwa kwenye kiwango bora kabla ya Yanga kusawazisha dakika ya 115 kupitia Denis Nkane na kufanya dakika 120 ishirini kukamilika kwa sare ya 3-3.


Katika mikwaju ya penati Yanga ndio walikuwa bora wakipata penati nne kupitia Yannick Bangala, Dickoson Job, Heritier Makambo na Khakid Aucho huku Coastal wakipata moja kupitia Victor Akpan wakati Amani Kyata na Rashid Chambo wakikosa.

Mchezaji bora wa mchezo huo amechaguliwa kuwa Abdul Sopu ambaye ameweka rekodi kwa kufunga mabao matatu.

Mabadiliko kwa timu zote Yanga alitoka Chico Ushindi akaingia Heritier Makambo na Djuma Shaban ambaye nafasi yake ilichukuliwa na Kibwana Shomari kwa Coastal alitoka Mtenje Albano akaingia Pascal Kitenge na Gustava Lunkombi akaingia Rashid Chambo.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments