Ticker

6/recent/ticker-posts

Yanga yatoa sababu Morrison, Bangala kuchelewa kambini
UONGOZI wa Yanga umethibitisha kuchelewa kujiunga kwa mastaa wao wawili, Bernard Morrison na Yanick Bangala kutokana na sababu mbalimbali.

Yanga tayari wameanza mazoezi ya kujiweka fiti kujiandaa na msimu mpya wa ligi sambamba na mashindano ya kimataifa wakiiwakilisha nchi Klabu bingwa.

Akizungumza Dar es Salaam leo, Ofisa Habari wa klabu hiyo, Hassan Bumbuli alisema wachezaji wote wamewasili kambini isipokuwa Bangala na Morrison ambao hadi alhamisi watakuwa wameungana na wenzao kwenye mazoezi.

"Mastaa hao taarifa za kuchelewa kwao zinafahamika lakini wote watawasili kesho na alhamisi wataanza mazoezi pamoja na wenzao ili kujiweka witi kuelekea msimu mpya," alisema na kuongeza;


 
"Ni wachezaji watano ambao walichelewa kujiunga na kambi ambao ni Khalid Aucho ambaye jana kaanza mazoezi, Fiston Mayele na Shaban Djuma ambao wataanza mazoezi leo baada ya kuwasiri jana."

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments