Ticker

6/recent/ticker-posts

Yanga Yatwaa Ubingwa wa Shirikisho Kombe la ASFC kwa Mikwaju ya Penati lakini Huyu Soup Kawahenyesha

Abdul Suleiman Sopu amefunga mabao matatu kwenye mchezo dhidi ya Yanga
KLABU ya soka ya Yanga imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Shirikisho maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation Cup ikiwa ni baada ya kuifunga Coastal Union kwa changamoto ya mikwaju ya penati 4-1.

Mchezo ulilazimika kuamuliwa kwa changamoto ya mikwaju ya penati ikiwa ni baada ya timu zote mbili kulazimishana sare ya mabao 3-3 katika kipindi cha dakika 120 ambapo mabao ya Yanga yalifungwa na Feisal Salum, Herittier Makambo Pamoja na Denis Nkane huku yale ya Coastal Union yakifungwa na Abdul Suleiman Sopu aliyefunga mabao yote matatu yaani Hat Trick.


Feisal Salum Fei Toto akishangilia bao lake lililoirudisha Yanga mchezoni
Kwa ushindi huo Yanga inafanikiwa kumaliza msimu ikiwa haijapoteza mchezo hata mmoja katika mashindano yote ya ndani kwa maana ya ngao ya jamii, Ligi Kuu ya NBC Pamoja na Kombe la Shirikisho.


Herittier Makambo akiwajaza wananchi baada ya kufunga bao la pili kwa Yanga
Wachezaji wa Yanga waliopata mikwaju ya penati ni Yannick Bangala, Dickson Job, Herittier Makambo Pamoja na Khalid Aucho huku ile ya Coastal Union ikifungwa na Victor Akpan.


Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments