Ticker

6/recent/ticker-posts

Zimbabwe yatambulisha sarafu ya dhahabu

Benki Kuu nchini Zimbabwe imezindua sarafu za dhahabu katika juhudi za kupunguza mahitaji ya fedha za kigeni nchini humo pamoja na kukabiliana na mfumuko wa bei lakini wachumi na nchini humo wanatilia shaka jambo hili.

Katika uzinduzi rasmi wa sarafu za dhahabu mjini Harare mapema jana, John Mangudya, Mkuu wa Benki Kuu ya Zimbabwe amesema sarafu hizo zimezinduliwa ili kupunguza mahitaji ya dola za Marekani nchini humo.

Wazimbabwe kwa kiasi kikubwa wanaepuka sarafu za ndani ya nchi hiyo wakiipa kipaumbele dola ya kimarekani ambayo wanaona kuwa inakubalika zaidi nje ya nchi na kushikilia thamani yake kwa muda mrefu.

Mangudya amesema ana matumaini kwamba Wazimbabwe sasa watachagua sarafu za dhahabu, ambazo zinagharimu takriban dola 1,800 (Tsh. 4,196,700) kwa kila sarafu moja, sarafu 2,000 zitatengenezwa na uzalishaji wa baadae utategemea hamu na uhitaji wa wananchi.


 
Wananchi kutokea chini Zimbabwe wamelipokea hili suala kwa mashaka, wakisema mwananchi wa kawaida hatoweza kumudu gharama za sarafu hi, na kwamba imetengenezwa kwa Watu matajiri.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments