Zoran Maki Kabla Hujaanza Kazi SIMBA Mpigie Pablo Simu Umuombe Machozi yake


 
Zoran Maki umekuja kipindi ambacho bado machozi ya mashabiki wa Simba yanamwagika juu ya kidole cha mwisho cha mguu,umekuja kipindi ambacho mashabiki wa Yanga furaha yao inatembea kifua mbele,furaha yao ni muhimu kuliko maisha yao.

Ule mkataba wa mwaka mmoja uliopewa na Machifu wa msimbazi unaweza kukuvunja moyo unaweza kuwa tumaini jipya jambo la msingi muombe sana Mungu uwe na mwisho mwema maana mashabiki wa Simba sio waumini wa kushindwa aghalabu.

Zoran Maki una kazi ngumu ya kupandisha jiwe kubwa mlimani kwasababu kushinda ubingwa ligi kuu,kufika nusu ya caf Champions Leageu,na kushinda mataji mengine ya ndani sio sawa na uzito wa unyoya.

Zoran Maki kabla hujaanza kazi mpigie Pablo Franco simu muombe akupe machozi yake hakika utapata hekima kuhusu maisha ya soka la Tanzania hakika utafunza maana halisi ya kusimama mbele ya maghorofa ya Kariakoo macho yakitazama juu.

Karibu sana kocha wa mpira Zoran Maki.

@omarrkombo

💥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SERIKALINI

💥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SEKTA BINAFSI

💥NAFASI ZA INTERSHIP MAKAMPUNI MBALI MBALI

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. I did so many searches on this topic. As a result, this article is one of the top three articles I want to recommend to people. I have been in this field for years, so I know how accurate this article contains. If you are curious about the contents, please visit my blog anytime. 메이저토토Check out this

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad