Akianguka Kutoka Milima ya Montblanc

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPABINGWA wa kupanda milima na kuteleza kwenye theluji mwanadada Adele Milloz, 26, afariki dunia baada ya kuanguka kutoka safu za milima ya Montblanc nchini Ufaransa.

Milloz alikuwa ameachana na michezo ya kitaalamu na kuhamia kwenye uongozaji wa wapanda milima.

Yeye na mwenzi wake, walikuwa wakipanda Aiguille du Peigne, Ufaransa siku ya Ijumaa kabla ya tukio hilo kutokea.


Adele Milloz, 26 amefariki baada ya kudondoka kutoka mlimani
Wapanda milima wengine walishuhudia anguko hilo na wakapiga kelele, Huku chanzo hasa cha anguko hilo kikiwa bado hakijafahamika


Milloz alikuwa mpandaji mzoefu ambaye hapo awali alishindana katika upandaji milima wa skimo, ambao huusisha kupanda katika kilele cha mlima wenye barafu na kuteleza chini.

Milloz, ambaye alikulia huko Tignes katika Alps ya Ufaransa, alishinda ubingwa wa ulimwengu katika mchezo huo mnamo 2017, na Bingwa wa Uropa mnamo 2018.


Adele Milloz, bingwa wa kupanda milima kwa muda mrefu amefariki dunia
Waziri wa Ufaransa wa michezo na Michezo ya Olimpiki, Amélie Oudéa-Castéra


Alisema: “Nimehuzunishwa sana na kifo cha bingwa wa wapanda milima ya Ski, Milloz huko Mont Blanc, Natuma rambirambi zangu za dhati kwa familia yake, wapendwa wake na wafanyakazi wenzake kutoka umoja wa Kitaifa wa Utelezi na Kupanda Milima huko Chamonix.”
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad