Ticker

6/recent/ticker-posts

Bilionea wa Ukraine Auawa Katika Shambulio Lililotekelezwa na Urusi
BILIONEA maarufu nchini Ukraine Oleksiy Vadatursky ameuawa yeye pamoja na mke wake Raisa kufuatia shambulio lililotekelezwa na majeshi ya Urusi baada ya kombora kulipua nyumba yao wakati wamelala.

Vadatursky ni bilionea aliyekuwa akimiliki Nibulon, Kampuni inayohusika na usafirishaji wa nafaka ambaye hivi karibuni alitunukiwa tuzo ya heshima ya ushujaa kutoka kwa rais wan chi hiyo Volodymyr Zelensky.


Jengo la Bilionea aliyeuawa na majeshi ya Urusi akiwa pamoja na mke wake
Meya wa Jiji la Mykolaiv Oleksandr Senkevych amesema pengine shambulio hilo ndilo linaloweza kuwa moja ya mashambulio makubwa kuwahi kutokea katika Jiji hilo hadi sasa.

Shambulio hilo limesababisha uharibifu wa hoteli, viwanja vya mpira, Shule mbili pamoja na vituo vya mafuta.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments