Edo Kumwembe: Young Africans inanipa homa

 


Mwandishi wa Habari za Michezo Mwandamizi nchini Tanzania Edo Kumwembe ameonyesha Shauku ya kutaka kuiona safu ya Ushambuliaji ya Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans.


Safu ya Ushambuliaji ya Klabu hiyo Kongwe katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, inaundwa na Fiston Mayele, Heritier Makambo, Lazarius Kambole, Stephen Aziz Ki na Bernard Morrison.


Kumwembe ameonesha Shauku hiyo wakati akikichambua kikosi cha Young Africans kupitia Kipindi cha Sports Arena cha Wasafi FM, leo Ijumaa (Agosti 05).


Amesema kuna haja ya kila Mwanachana na Shabiki wa Young Africans kwenda kuitazama timu yake Kesho Jumamosi (Agosti 06), katika mchezo wa Kirafiki dhidi ya Mabingwa wa Uganda Vipers SC, ikiwa ni sehemu ya Shamra Shamra za Siku ya Wananchi, Uwanja wa Benjamin Mkapa.


“Ukiwa shabiki wa Mwananchi na ni katika WIKI YA MWANANCHI ni wakati mzuri kuwatazama Aziz Ki, Fiston Mayele na Bernard Morrison wakicheza pamoja kulisaka lango la wapinzani….usikae home. Hii safu inanipa kahoma flani hivi”


Young Africans itautumia mchezo dhidi ya Vipres SC kama sehemu ya kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba SC, utakaopigwa Jumamosi (Agosti 13), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad