Harmonize Amtoa Kizz Daniel Lupango Osterbay


Hatimaye mwimbaji wa muziki kutoka Nigeria, Kizz Daniel ametolewa katika kituo cha Polisi
cha Oysterbay jijini Dar es salaam alipokuwa amewekwa rumande. Msanii @harmonize_tz amemtoa mikononi mwa Polisi usiku huu na kuondoka nae.

Tukio hilo ambalo limeshuhudiwa na Bongo5, wameripoti kuwa, @harmonize_tz alifika kituoni hapo tangu majira ya saa 2 usiku na kutumia muda wa takribani saa moja na nusu kufanya mazungumzo na askari kituoni hapo na baadaye kuondoka na msanii huyo.

Itakumbukwa, mapema leo majira ya saa 10 alasiri, Kizz Daniel alikamatwa na kuwekwa rumande katika kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar es salaam, hii ni baada ya kushindwa kutokea kwenye show ya Summer Amplified aliyotakiwa kutumbuiza usiku wa kuamkia leo.💥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SERIKALINI

💥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SEKTA BINAFSI

💥NAFASI ZA INTERSHIP MAKAMPUNI MBALI MBALI

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad