Irene Uwoya "Sitaki Kujitia Gundu"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Irene Pancras Uwoya au Mama Krish; ni nembo ya tasnia ya Bongo Movies ambaye anasema kuwa, katika maisha yake hataki kujitia kero na gundu.

Uwoya anasema kuwa, kwa sasa mtu akijitia kero ni kujitakia mwenyewe kwa sababu kuna vitu vingi mno vya kumpa mtu furaha kila siku na siyo kero.

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Uwoya anasema kuwa, alishasahau kero kitambo na ndiyo maana siku hizi anaachia nafsi yake kuwa na furaha tu na si kitu kingine.

Anasema hii ndiyo maana hivi karibuni aliamua kutafuta mtu wa kumchekesha ili roho yake ifurahi.

“Mimi sitaki kero wala kujitia gundu kwa kuwaza chochote kwenye maisha yangu haya hata siku moja.

“Hii ni kwa sababu sitaki kuyatia gundu maisha yangu hata kidogo, mimi nahitaji raha siyo karaha,” anasema Uwoya ambaye kwa sasa ndiye staa wa kike mwenye mkwanja mrefu Bongo nzima.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad