Kimeumana: Chebukati Afichua Alionywa Dhidi ya Kutangaza Ruto Mshindi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC Wafula Chebukati amesema alikuwa ameonywa dhidi ya kumtangaza William Ruto mshindi wa urais.


Wafula Chebukati alisema alikuwa ameonywa dhidi ya kumtangaza William Ruto kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais. Chanzo: UGC
Kwa mujibu wa Chebukati, kikosi kutoka kamati ya kushauri rais kuhusu usalama (NSAC) ilifika Bomas na kutoa msimamo huo.

Wakiongozwa inspekta jenerali wa polisi Hillary Mutyambai, Wakili mkuu Kennedy Ogeto, naibu mkuu wa jeshi Omondi Ogola na katibu mratibu katika afisi ya rais Kennedy Kihara, maafisa hao walisema itakuwa kosa kubwa Ruto kushinda uchaguzi.


Hilo lilikuwa likifanyika saa nane mchana Agosti 15 huku Kihara akiambia Chebukati kuwa nchi itachomeka iwapo Ruto atatangazwa mshindi.


"Kihara aliendelea kutuonya kuwa iwapo tutatangaza matokeo jinsi yalivyokuwa ambapo Ruto alikuwa mshindi na vurugu kuzuka, basi damu ya Wakenya ambao watauawa itakuwa mikononi mwetu," Chebukati anasema kwenye kiapo chake mahakamani.

Ni masuala mazito ambayo yanazidi kuibuka katika kesi ya Azimio mahakamani huku IEBC wakiamua kuchomeana.

Katika kiapo cha kamishna Abdi Guliye, alisema baada ya kikosi hicho cha usalama kuondoka, Chebukati aliwataka kutoa maoni yao.

Makamishna Juliana Cherera, Justus Nyang'aya, Iren Masit na Francis Wanderi ndio walikuwa wa kwanza kuchangia.


Walisema ushauri wa kikosi hicho cha usalama ni muhimu na hivyo IEBC ilifaa kukarabati hesabu ili mambo kuingiana.

Ni wazi kuwa itakuwa hali ya nipe nikupe katika mahakama ya Upeo huku kila pande ikijaribu kuanika wenzao.

Raila Odinga ndiye alifika mahakamani akitaka ushindi wa Ruto kutupiliwa mbali na yeye kutangazwa mshindi.


Majaji saba wanatarajiwa kutoa uamuzi kuhusu kesi hiyo ifikapo Septemba 5.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad