Ticker

6/recent/ticker-posts

Mfalme Zumaridi abadilishiwa HakimuBaada ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Monica Ndyekobora, wa Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mwanza, kugoma kujitoa kusikiliza kesi ya Diana Bundala maarufu kama Mfalme Zumaridi na wafuasi wake 84, hatimaye Mahakama hiyo imempangia Hakimu mwingine kusikiliza kesi hiyo.
Mawakili wa upande wa utetezi walitaka kuwasilisha hoja za mteja wao Zumaridi kutokuwa na imani na Hakimu aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo lakini kutokana na Mahakama hiyo kuamua kupanga kesi hiyo kwa Hakimu mwingine wakaona hakuna haja ya kuwasilisha hoja hizo

Wakili upande wa serikali Emmanuel Luvinga, ameiambia Mahakama hiyo kuwa kutokana na upande wa utetezi kusema watawasilisha hoja hizo leo hawakuweza kuwaleta mashahidi mahakamani, hivyo kuomba kesi hiyo ambayo inasikilizwa na Hakimu mkazi Clesensia Mushi ipangiwe tarehe nyingine

Akizungumza nje ya Mahakama wakili wa utetezi Linus Amri, ameshukuru uamuzi huo wa Mahakama wa kubadilisha Hakimu.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments