Mfuasi wa Mfalme Zumaridi amkaanga kortini

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




MSHTAKIWA namba 17, Hildegard Stanslausi katika kesi ya jinai namba 12 ya mwaka 2022 inayomkabili Mchungaji Diana Bundala maarufu Mfalme Zumaridi mkazi wa jijini Mwanza na wenzake  84  amejikuta katika wakati mgumu...

...baada ya kukiri mahakamani shtaka lake la kushambulia maofisa wa umma na kuwasababishia majeraha.

Stanslausi, baada ya kukiri kosa hilo,  Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza, Crescensia  Mushi aliamua kutumia busara na kuahirisha kesi hiyo kwa saa moja ili kumpa nafasi mshtakiwa kufiria alichokijibu.

Tukio hilo lilitokea leo katika mahakama hiyo baada ya mshitakiwa kusomewa kosa lake na hakimu kumtaka aseme ndiyo kama alifanya ama aseme hapana kama hakufanya, yeye akasema ndiyo, akimaanisha alifanya kosa hilo.

Mshtakiwa huyo alikiri kosa lake na kuiambia mahakama kwamba siku ya tukio akiwa na waumini wenzake walishirikiana kuwaita na kuwachokoza askari na kisha kuanza kuwashambulia.

Baada ya maelezo hayo mahakamani kulizuka sintofahamu baada ya  mshtakiwa namba moja, Mchungaji  Diana Bundala (Mfalme Zumaridi),  kupaza sauti ya juu ndani ya mahakama kumtaka mtuhumiwa huyo kukana kosa.

Imeandikwa na Vitus  Audax  na Pelusy  Yohana (SAUT)
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad