Ticker

6/recent/ticker-posts

Mkewe Chameleone Atoa Ushahidi wa Kutisha Kuthibitisha Shemejiye Weasel amekuwa Akimdhulumu MkeweWiki iliyopita, moja ya habari zinazovuma zaidi kwenye mitandao ya kijamii nchini Uganda ni madai ya mwimbaji maarufu Weasel Manizo kumshambulia na kumdhulumu mkewe Sandra Teta.

Picha zilizomuonyesha Sandra akiwa amevimba na kuchubuka usoni zilisambazwa kote mitandaoni sambamba na uvumi kuwa anaendelea kupata afueni nyumbani baada ya kupigwa vibaya na mwanamuziki huyo.

"Mwimbaji Weasel anaripotiwa kumpiga mpenzi wake Sandra Teta. Kwa sasa anauguza majeraha," Ripoti ya kituo kimoja cha habari nchini Uganda ilisoma.


Bi Sandra hata hivyo alijitokeza kupuuzilia mbali madai ya kupigwa na mumewe na badala yake kudai alikuwa ameshambuliwa na majambazi wakati akielekea nyumbani mnamo Julai 22, 2022 usiku.

"Kwa kurejelea picha zilizosambaa kwenye Vyombo vya Habari, nikiwa njiani kutoka kazini Ijumaa usiku, nilivamiwa na majambazi wasiojulikana ambao walikimbia na simu yangu, mkoba na Ush1.3M. Kwa muda wa wiki moja iliyopita nimekuwa kwenye matibabu na ninaendelea kupata nafuu," Teta alisema kupitia Instagram.

Weasel ambaye ni kakake Chameleone aliunga mkono kauli ya mkewe na kubainisha kuwa alikuwa akipata afueni nyumbani.

Mkewe Chameleone, Daniella Atim, hata hivyo amesisitiza kuwa shemeji huyo wake ana tatizo na amekuwa akimnyanyasa mkewe kimwili.


Daniella kupitia ukurasa wake wa Instagram alitoa ushahidi mpya kuhusu shambulio la awali la Weasel kwa mkewe. Alidokeza kuwa Bi Sandra bado hajaweza kupata ujasiri wa kuzungumzia masaibu anayopitia nyumbani.

"Hizi ni picha za Sandra za mwezi Desemba ;Sandra anahitaji msaada wetu sote, kwa namna yoyote ile .Anahitaji sisi sote kupaza sauti zetu ili kumsaidia katika jambo la kwanza muhimu zaidi, kujiamini kwake. Sote tuweke uzito nyuma ya Sandra na tumsaidie kutembea safari hii," Daniella aliandika chini ya picha za kutia huruma za mkewe Weasel.

Katika picha hizo, Bi Sandra alionekana kuwa na michibuko mwili mzima ikiwa na pamoja na kwenye shingo, mgongo, makwapa na magoti yake.

Daniella alitoa wito kwa wanawake na wanamitandao wengine kusaidia kumwokoa mwanasoshalaiti huyo wa Rwanda kutoka 'jela' aliyomo sasa.


"Watoto wa Sandra wanastahili bora zaidi!" Alisema.

Katika chapisho lingine, mkewe Chameleone alidokeza kuwa watoto wa shemejiye wanaumia sana kufuatia mzozo kati ya wazazi wao.

"Hawa ni watoto wa Sandra wakitupwa nje ya eneo lake la kazi. Kimila watoto hawa pia ni watoto wangu. Je, huwa tunasimama kwa sekunde moja na kufikiria jinsi tukio hili litakuwa na athari kwa watoto hawa wasio na hatia miaka 10-20 kutoka sasa?" Daniella aliandika chini ya picha zilizoonyesha watoto wa Weasel wakiwa wameachwa nje ya lango huku wakionekana wenye huzuni kubwa.

Daniella alitoa wito kwa Weasel kusaidiwa kupambana na hali inayomuathiri, Sandra kupata haki na watoto wao kulindwa .

Weasel na Bi Sandra walianza kuchumbiana mwaka wa 2018 na tayari wako na watoto wawili pamoja.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments