Ticker

6/recent/ticker-posts

Rais Samia: Chalamila we ni Mtundu sana, Natumaini Umekua Sasa
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemuasa Mkuu mpya wa Mkoa wa Kagera Albert Chalamila kuwa aache utundu na hatimaye ajikite katika kutekeleza amajukumu yake mapya kama Mkuu wa Mkoa.

 

Rais Samia ameyasema hay oleo Agosti 1, 2022 katika Hafla ya Uapisho wa Viongozi mbalimbali wateule uliofanyika Ikulu ya Dar es Salaam.


Wakuu wapya wa Mikoa ambao ni wanajeshi wameelekezwa kutovaa mavazi ya kijeshi wakiwa katika majukumu yako kama wakuu wa Mikoa

“Mwanangu Chalamila mategemeo yangu umekua sasa, akili imetulia, wewe ni mfanyakazi mzuri lakini mtundu mno, sasa nilikuacha nje kipindi hicho lakini nimeamua kukurudisha naomba ukakue, ukue akili itulie uende ukafanye kazi ukanisaidie eneo ulilopangiwa, wala hii haina maana kwamba ndiyo umemaliza ukikaa hapo umekaa nakuangalia kwa karibu sana.” Amesema Rais Samia.


Aidha Rais Samia amebainisha kuwa waliokuwa wakuu wa Mikoa ambao walikuwa ni wanajeshi amewarudisha Jeshini kutokana na wao kuhitajika kwenda kufanya kazi jeshini na amewapandisha vyeo cha Meja Jenerali.

 

Lakini pia Rais Samia amewasisitiza wakuu wapya hao wa Mkoa kutovaa mavazi ya Kijeshi wanapokwenda kuwahudumia wananchi watavaa nguo zao za kijeshi mara majukumu yao ya Ukuu wa Mkoa yatakapotamatika.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments