Rais Samia: Kwa Upande wa Mafuta Mpaka Huko Duniani Waache KupiganaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiongea na wananchi wa Mbalizi mkoani Mbeya
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kuwa kwa tatizo la mafuta nchini kuweza kutatuliwa ni mpaka nchini kubwa barani Ulaya ziache kupigana.

Rais Samia ameyasema hayo wakati akiongea na wananchi wa Mbalizi mkoani Mbeya ambapo yupo kwa ajili ya ziara ya kikazi ikiwemo kuzindua mradi wa maji mkoani humo.


Rais Samia Suluhu Hassan
Rais Samia amenukuliwa akisema:

“Kwahiyo kwa upande wa mafuta ni mpaka huko duniani waache kupigana, mpaka huko duniani bei zianze kushuka ndiyo tutapata unafuu vinginevyo zile pesa mnazodai za barabara, vituo vya afya na umeme itabidi tukate tupeleke ruzuku kwenye mafuta kuzuia bei isipande.”


Rais Samia amesema ili bei ya mafuta ipungue ni hadi mataifa ya Ulaya yaache kupigana
Aidha Rais Samia amewakumbusha wananchi kuwa Serikali inaweza kiasi cha Bilioni 100 kila mwezi kama ruzuku ili kusaidia kupunguza gharama za bei za mafuta nchini.

______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad