Rommy Jones Aanika Kuhusu Picha Zake za Utupu, Aomba Radhi kwa Watanzania

 


KAKA wa Msanii Diamond Platnumz, Rommy Jones almaarufu RJ the DJ kwa mara ya kwanza amefunguka kuhusu sakata la picha za utupu wake kuvujishwa mitandaoni na mwanaharakati mmoja wa kimitandao kupitia ‘app’ yake.


RJ amechukua fursa hiyo pia kuwaomba radhi mashabiki zake na wote waliokwazika na kitendo hicho akisema kwamba hajui zilimfikiaje mwanaharakati huyo ila anahisi ni fundi wa simu alizivujisha baada ya kumpelekea simu kuitengeneza.


“Zile picha zilizovujishwa na … (anamtaja) ni za muda mrefu, nilirekodi nilikuwa nimelewa na sijui nani aliamua kuzivujisha. Kuna mtu alipigia simu miaka mitatu minne nyuma alinipigia akaniambia: “Nina picha zako za utupu, ili nisizisambaze nitumie milioni moja nizifute”, mimi nikashtuka nikamwambia sina pesa.


“Ile simu niliyokuwa natumia mwanzo iliharibika nikaipeleka kwa fundi ili aitengeneze, ni rafiki yangu yupo Mwenge, baada ya jamaa yule kunitumia picha zile nikaripoti Polisi Oysterbay nikapewa RB, akawa anatafutwa mara yuko Buguruni mara yupo Mbezi.


“Baadaye akanitumia zile picha, ikabidi nimtumie mke wangu kumuuliza kama kwenye simu kuna hizo picha akakataa, nikamcheki fundi wangu kumuuliza kama ile simu ameiuza akasema hapana ila amei-flash, nikaenda kwake nikahakikisha kweli ame-flash hakuna picha yoyote,” RJ the DJ alisema.

Rommy amewaomba radhi wote kuanzia familia yake ambayo ni mke wake, ndugu zake na pia mashabiki wa Wasafi kwa kitendo hicho.


“Nichukue fursa hii kuomba msamaha kwa Mungu, mke wangu, familia yangu pamoja na mashabiki wangu wote haijalishi yalikuwa ya kweli au ya uongo,” alisema Rommy.


Vilevile, msanii huyo alitumia fursa hiyo kufunguka siri za kudumu kwa ndoa yake ambayo imedumu muda mrefu.


“Mara nyingi ndoa zinazodumu kwa muda mrefu ni zile ndoa ambazo nakwambia… mimi nataka kukuoa, kwa sababu mimi ndio mwanaume ninayeshikilia mahusiano yetu pia nashikilia familia yetu.


“Wewe ukiniambia tuoane kwa sababu labda umeona shoga zako wanaolewa au ndugu zako wanasema huyu mwanaume mbona hakuoi umekaa naye muda mrefu, hapo utataka uolewe na mimi kwa sababu ya shinikizo.


“Mimi mke wangu hakuniambia tuoane bali mimi ndiyo nlimwambia tuoane kwa sababu mimi nlikuwa nipo tayari na ndio maana mpaka Sasa ndoa ipo,” alisema DJ.


Usiku wa kuamkia jana, Rommy Jones ameshinda tuzo ya Dj Bora Afrika Mashariki katika tuzo za @aeau_awards.

______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad