Ticker

6/recent/ticker-posts

Simba itakavyovuna mabilioni yake...KLABU ya Simba imesaini mkataba wa udhamini mkuu na kampuni ya M-Bet wa miaka mitano ukiwa na thamani ya Shilingi 26.1 bilioni.

Simba mgawanyo wake kwa miaka mitano mwaka wa kwanza ni Sh4.670 bilioni, mwaka wa pili Sh4.923 bilioni , mwaka wa tatu Sh5.205 bilioni, mwaka wa nne Sh5.205 bilioni na mwaka wa tano ni Sh5.853 bilioni.

Akizungumzia mkataba huo, Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya M-Bet, Allan Mushi amesema kusaini mkataba wa kuidhamini klabu ya Simba haikuwa rahisi.

Mushi amesema iliwachukua muda mrefu kukubaliana baadhi ya vipengele kwani vipo ambavyo Simba ilikuwa inavitaka na vingine wao walikuwa wanataka vikae sawa.

“Tupo Simba kutokana na mafanikio yao kwenye Ligi ikichukua ubingwa na kufanya vizuri nje kuitangaza Tanzania, sisi pia hatupo Tanzania pekee na ndio maana tukaona tuweke nguvu hapa,” amesema na kuongeza

 "Baada ya mkataba huu tunaweza tukaendelea kuwa hapa kwa sababu sisi na Simba tunafanana mpaka rangi.”

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments