Simba SC yafunguka sakata la JEZI mpya
Huenda Mashabiki wa Klabu ya Simba wakakosa nafasi ya kuwa na Jezi maalum wakati wa Tamasha la Simba ‘Simba Day’ siku ya Jumatatu ‘Agosti 08’ Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Hadi sasa Simba SC haijatambulisha jezi mpya za Msimu ujao wa Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho na Michuano ya Kimataifa inayoratibiwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’.

Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amesema hadi sasa klabu hiyo pamoja na Mbunifu na Muuzaji Rasmi wa Vifaa vya Michezo vya Klabu hiyo kampuni ya Vunja Bei wanaendelea kupambana na changamoto ambazo zimesababisha jezi za msimu ujao kutoka kwa wakati.

Ahmed Ally ameweka wazi suala hilo alipofanyiwa mahojiano na Kituo cha Wasafi FM, leo Ijumaa ‘Agosti 08’ kupitia Kipindi cha Sports Arena kilichorushwa asubuhi.


 
“Jezi hazijazuiwa bandarini na (TBS) kwa sababu ya ubora hafifu wala si kwa sababu wameshindwa kuzilipia kodi kama baadhi ya watu wanavyosema,”

“Sio kawaida na sio sawa kutokutangaza Jezi zetu mpaka Leo! Kuna kitu kisichokuwa cha kawaida kimesababisha kuchelewa na sio kwamba zimekwama bandarini”

“Mabadiliko ya Mdhamini mchakato ulianza mwezi wa 6 ukachukua muda, mnakubaliana lakini kesho mdhamini anaibuka na mawazo mengine.”


“Kama tungebaki na mdhamini aliyepita tungekuwa na Jezi mpya mapema sana” amesema Ahmed.
______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad