AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA
MWIMBAJI na mwanamitindo maarufu nchini Kenya, Tanasha Donna ameweka wazi kuwa kwa sasa hana mpenzi.
Tanasha ambaye ni mzazi mwenzake na Diamond Platnumz amesema kuwa yuko tayari kumpa mwanaume mwingine nafasi katika moyo wake.
"Nipo single! Labda kuna mtu ambaye anaweza kuwa mpenzi anayefuata, inaweza kuwa," amesema Tanasha.
Mama huyo wa mtoto mmoja alibainisha kuwa hazingatii sura ya mwanaume wala utajiri wake anapotafuta mchumba.
Alifichua kuwa jambo la msingi analozingatia kwa mwanamume anayekusudia kuchumbiana naye ni tabia yake.
"Tabia ni muhimu sana kwangu. Ni ufunguo wa kila kitu maishani kwa sasa kando na Mungu, mimi ni muumini pia," alisema.
Tanasha pia alidokeza kuwa mwanaume anayetazamia kuchumbiana naye ni sharti awe mwenye bidii na mcha Mungu.
NAFASI ZA AJIRA
JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA
GOODLUCK