Ticker

6/recent/ticker-posts

Uhuru Atangaza Urais wa Raila Odinga "Ruto Subiri Fursa Nyingine"Rais Uhuru Kenyatta amempa ukweli naibu wake William Ruto, kuwa aache kueneza uongo kwa Wakenya kwamba Kenyatta alimtendea mabaya wakati wa uongozi.

Akizungumza katika Kaunti ya Mombasa siku ya Alhamisi, wakati wa uzinduzi wa miradi ya miundomsingi, Uhuru alisema Kenya haina haja na kiongozi anayewahadaa.

Ameyasema hayo alipokuwa akiyajibu madai ya Ruto kwamba serikali ya Jubilee, ilifeli katika muhula wake wa pili, kwa kushindwa kukamilisha miradi ya maendeleo, kufuatia handshake na kinara wa ODM Raila Odinga.

Uhuru alisema kwamba Raila ndiye anayefaa kuwa mrithi wake, na kumshauri Ruto kusubiri fursa nyingine ya kuwania urais.


“Ninasikia wakisema kwamba miradi ya serikali ilikamilika mwaka wa 2018 wakati wa handshake na kakangu Raila. Wacha niwaulize, huu mradi tunaouzindua leo, tulizindua 2020, sasa ilikuwa ni baada au kabla ya handshake? Kwani hii sio kazi tumefanya? Tunahitaji serikali itakayowaunganisha Wakenya wote, kwa hiyo mruhusu Raila aingie ili aweze kufanya kazi, wengine wasubiri fursa nyingine wakati mwingine,” alisema Rais Kenyatta.

Katika hatua nyingine Naibu rais William Ruto amemtaka Rais Uhuru Kenyatta kuhakikisha kuwa taifa liko salama wakati huu wa uchaguzi mkuu kwa kutuliza wanaopanga kuzua chuki za kisiasa kipindi hiki.

Ruto amesema baadhi ya maafisa wa serikali wanafanya siasa mbaya katika juhudi za kumuuza mgombea wa Azimio Raila Odinga.


Alisema ni wakati serikali ikubali kuwa Raila hawezi kushinda uchaguzi wa urais na hivyo kuacha Wakenya kuamua nani anawafaa kwa Uongozi wa Nchi hiyo.

Ruto alisema woga umewaingia Azimio kiwango cha kutaka kucheza michezo ya michafu hali ambayo inahatarisha maisha ya Wakenya.

“Ile wasiwasi tunaona Azimio haitawasaidia. Kile tunamuomba Rais, kwa heshima, ni asiruhusu nchi kupatwa na chuki za kisiasa hata kama project yake imeanguka. Hakuna haja ya kuanza kueneza chuki,” alisema Ruto.

Kenya inatarajiwa kufanya uchaguzi wake mkuu Agosti 9, 2022 ili kumpata mrithi wa Rais wa sasa Uhuru Kenyatta ambaye ameongoza nchi kwa mihula miwili.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments